Machapisho

Sifa za Mwanaume wa Ukweli Chini ya Jua !

Picha
SIFA YA MWANAUME WA UKWELI, SI KUWA NA VIBINTI, VIBICHI VIBICHI, BALI TUTAKUPIMA KATIKA MAMBO YAFUATAYO ! Ujanja wa mwanaume si kujua kutongoza wasichana. Imekuwa kama kadesturi miongoni mwa vijana tuliowengi ,tulioibukia katika kizazi hiki kinachoifahamu computer kuliko kitu kingine. Kizazi kichoifahamu Google kuliko mlango wa kanisa au msikiti inashangaza.Mithili ya watu tuamkao toka usingizini tumepigwa na butwaa na bumbuazi limetuenea mawazoni hatuna cha kusema mbele ya dunia ya mavumbuzi. Tumeshindwa kujiongoza,tumeyakubali matakwa ya mwili pamoja na tamaa iongoze mstakabari wa maisha yetu. Tumeona ni ni ujanja na ufahari kuwa na mademu wengi,kuliko kuhangaikia mambo ya msingi kwa ajili ya kesho inayo kuja mithili ya upepo wa kimbunga. Tumekuwa washamba wa mapenzi na ulimbukeni usio na sababu ndio unao tuliza kila iitwapo Leo kwa sababu tumeingia kichwa kichwa katika mapenzi tukidhani ni kama kunywa chai, kumbe tumejipeleka vitanzini kwa hiari. Amakweli si kila anayejiita”born...

Vigezo 7 Vya Uchumba Wenye Mafanikio !

Picha
Je,Uhusiano wenu Unastahili kuitwa Uchumba?    Hakuna anayetazamia kuingia katika mahusiano ya kinafiki. Kila mtu anatamani kuwa na mtu sahihi,mwenye upendo wa kweli.Hakuna mwanadamu hata mmoja asiyehitaji kupendwa. kila kiumbe kinahitaji kupendwa,hii inaweza kushuhudiwa hata miongoni mwa wanyama tunao wafuga majumbani. Kila kijana anaye tazamia kuingia katika ndoa Siku moja, hana budi kujifunza kwa uangalifu kuhusiana na uchumba,urafiki na ndoa. Usifurahie kuambiwa neno nakupenda,maana si kila neno nakupenda linaashiria upendo wa kweli. Hata hivyo si kila mwanaume au mwanamke anafaa kuwa mwenzi wako.Mahusiano ya kimapenzi ni zaidi ya mwonekano wa kijinsia. Ni dhahiri tupo katika kizazi ,kijuaji,kikaidi na kisichopenda kusikiliza MASHAURI,omba usiwe wewe. Kila MTU mbishi atavuna mavuno ya ukaidi wake, hasa majuto.Kama jambo hulielewi,tafuta kijifunza jambo hilo.Epuka kuishi kwa kiyabahatisha maisha. Linapo kuja swala la mapenzi huna budi kujiuliza maswali,mengi kukuhusu.Ji...

Siri ya Mapenzi Yenye Kudumu !

Picha
Wapenzi hawana budi kuelewa hisia zao. Mapenzi yanayodumu ni Yale ambayo wapenzi wanaishi kama marafiki. Kama utabahatika kupata mpenzi ambaye ndiye aliye kuwa RAFIKI yako,utakuwa sehemu sahihi zaidi kupita wale tunaovamia mapenzi. Jifunze kupenda,hata kama hujawahi kupenda.Hii inaweza kusaidia namna ya kujali hisia za mwenzi wako,pamoja na mihemko yake na namna ya kuendana nayo pasipo shida yoyote. Ufundishe moyo wako namna ya kuitikia miali ya hisia zilizo ndani ya vilindi Vya moyo uliopenda. Tambua kuwa mwenzi wako ni wa thamani na thamani yake hakuna awezaye kuifikia,hivyo ni budi thamani,uzuri na upekee huo udumishwe ili kutoihafifisha thamani hiyo. Hakikisha tabasamu haliondoki machoni pa mpenzi wako,mfanye ajisikie mwenye bahati kuwa nawe.Waweza kumpatia ZAWADI,maneno matamu na kwa ukarimu wa dhati na kumfanya ahisi kana kwamba yupo katika jumba la kifalme. Usifanye choyo,kwa kumbania mpenzi wako.Kaa karibu naye uakisi hisia zake na upendo toka kwake. Epuka kuwa mzigo kwa mp...

Viungo 5 Murwaaa katika Ndoa !

Picha
Na:HekimaI.Luvanda Ili pilau la sikukuu linoge halina budi lipikwe kwa ufundi na maujuzi mengi,bila hivyo pamoja na hamu ambayo wanafamilia watakuwa nayo ujue fika hakuna atakaye thubutu kulisogelea pilau hilo ikiwa halijawekewa nakishi nakishi za kupendeza. Katika hali hiyo hiyo wanandoa hawana budi kufahamu wajibu wao wawapo katika ndoa. Nakupendekezea viungo muhimu sana katika ndoa yako ambavyo kupitia hivyo waweza kuponya ndoa yako. Viungo hivyo ambavyo nakupendekezea ndugu msomaji ni ; ASANTE MPENZI WANGU Hivi utapungukiwa nini kama utamwambia mpenzi wako asante kwa hicho kidogo alicho kupatia? Ujue wakati mwingine ni ujinga wetu tu....hata tunajikuta katika majanga.Kuna watu ili washukuru wanataka wapewe magari kama Rambo guene ndipo waseme asante. Je unajua kuwa zawadi ya ua ina maana kubwa kuliko vile unavyo Dhani? Jifunze kushukuru kikubwa hata kidogo pia. POLE MPENZI WANGU Mpe pole mpenzi wako kwa kazi na shughuli za kutwa.Usiu nyime haja yake moyo wako. Jisikie amani na ...

Majibu 4 yenye manufaa katika Maisha yako ya Mahusiano!

Picha
Na:HekimaI.Luvanda. Kwa kila anayetazamia kuwa na maisha yenye furaha katika ndoa yake,au maisha ya uchumba hana budi kujifunza majibu manne yenye maaana kubwa katika maisha ya mapenzi! Nakupendekezea mjibu manne; JIFUNZE KUSEMA NDIYO Ndiyo..yako iwe ni hakika katika kila utakalo lifanya.Hebu jifunze kusema ndiyo kama kweli unamaanisha hicho ukisemacho. Usiogope kusema ndiyo kama kweli moyo wako na nafsi yako vinakuambia hivyo. Dàima epuka unafiki katika maisha yako. Kuna mtu amewahi kusema ...ikiwa unasema ndiyo basi iwe ni ndiyo kubwa. Usione haya kumweleza mwenzi wako kilichopo moyoni mwako. JIFUNZE KUSEMA HAPANA Kwa hapana yako pia yaweza kubadili mwelekeo mbaya ambao huenda ungeathili maisha yako. Hapana , hapana ...kwa kile nisichokitaka kwanini niumie kwasababu ya mtu fulani asiye na huruma na maisha yangu? Tumia jibu la hapana pale inapobidi; Ukikasirishwa sema hapana Ukiumizwa sema hapana kwa hilo Ukifanyiwa jambo lolote lisilokupendeza usione Shaka kusema hapana pale usipo ...